Ndugu zangu leo tunawaletea neno fupi kabisa lakini lafaa katika maisha ya kiroho. Endelea kufuatilia kula siku:
Kufunga nini na inamaana gani katika maisha ya kiroho? imeandikwa 2Mambo
ya nyakati 20:3 "Yehoshefati akaogopa, akauwelekeza uso wake amtafute
Bwana akatangaza mbiu ya watu kufunga katika yuda yote."
Kufunga kunaonyesha hitaji letu kuu kwa Mungu imeandikwa Ezra 8:21
"Ndipo nikaamuru kufunga hapo penye mto Ahava ilitupatekujinyenyekeza
mbele za Mungu na kutafuta kwake njia iliyonyoka, kwa ajili ya sisi
wenyewe na kwaajili ya watoto wetu, na kwa mali yetu yote."
Kufunga kusifanywe ili kujionyesha imeandikwa Mathayo 6:17-18 "Bali wewe
ufungapo, jipake mafuta kichwani unawe uso; ili usionekane na mtu kuwa
unafunga, ila na BABA yako aliye sirini na BABA yako aonaye sirini
atakujazi."
Waweza kula chakula kido wakati unafunaga. imeandikwa Danieli 10:2, 3
"Katika siku zile mimi danieli nilikuwa nikiomboleza munda wa majuma
matatu kamili sikula chakula kitamu wa nyama wala divai haikuingia
kunywani mwangu wala sikujipaka mafuta kabisa hata majuma matatu
yalipotimia."
Na Mgalula Y Joseph
0752601632/0655601632