TEMBELEA KILA WAKATI UPATE HABARI ZA KUKUJENGA KIMWILI NA KIROHO PIA, PAMOJA TUNAJENGA MWILI WA KRISTO NA KWA NENO LAKE TUNAISHI MAANA KUISHI KWETU NI KRISTO BALI KUFA KWETU NI FAIDA ASEMA BWANA WA MAJESHI.
Tuesday, 25 June 2013
SEHEMU YA PILI (2)
4. ROHO MTAKATIFU ROHO ATUPAYE UTAKASO
Baada ya kuokolewa,tunahitaji pia kutakaswa.Bila utakaso,tutajikuta bado hatuna ushindi dhidi ya dhambi
za ndani katika mawazo,na moyoni,ingawa tayari tuna ushindi dhidi ya dhambi za kutenda.Dhambi za ndani
,ni kama hasira,wivu,chuki,masengenyo,kugombania ukubwa,kiburi,majivuno,kutokusamehe,kinyongo,
kupenda udunia n.k.Hivi vinaweza vikaonekana kwa watu waliookoka ambao hawajatakaswa:Mawazo
yasiyo ya ki Mungu (Mathayo 16:21-23),kugombania ukubwa (Luka 22:24-26;Mathayo 20:20-22,25-28;
Marko 9:30-37),hasira (Mathayo 20:24)wivu,fitina,ugomvi (Marko 9:38-39;Luka 9:49-50;
1Wakorintho 3:3-5),faraka na matengano(1Wakorintho1:10-13),umimi(Mathayo 28:6-13),
kutokusamehe(Mathayo 18:21-35),chuki,kushindwa kuvumilia maudhi,kushtakiana wapendwa mahakamani
(Luka 9:51-56;1Wakorintho 6:1-8);Warumi 7:15 n.k .Mambo haya huondolewa kwa utakaso.
Ndiyo maana Yesu aliwaombea Utakaso wanafunzi wake waliokuwa tayari wameokoka(Yohana 17:14-19)
Roho Mtakatifu ndiye atupaye Utakaso(1Wakorintho 6:11;1Petro1:2)Je,hujatakaswa,mwambie
Roho Mtakatifu akutakase,yeye ni mwaminifu,atafanya(1Thesalonike 5:23-24)
5. ROHO MTAKATIFU, ROHO ATUPAYE TUNDA LA ROHO
Katika Wagalatia 5:22-23,tunajifunza juu ya tunda la Roho.Katika lugha ya asili,yote katika mistari hii
yanamaanisha kwamba Tunda la Roho ni moja tu,Upendo.Hata hivyo,upendo huo unadhihirishwa kwetu
katika tabia na matendo kama furaha,amani,uvumilivu,utu wema,fadhili,imani,upole,na kiasi.Ni pale tu
tunapokuwa na maisha yaliyojaa upendo,ndipo tunapokuwa tunatimiza mapenzi ya Mungu katika maisha yetu.
Pasipo upendo,tunakuwa shaba iliayo na upatu uvumao,tunakuwa si kitu.Lolote jingine tunalolifanya linakuwa
halina faida(1Wakorintho 13:3).Hatuwi wanafunzi wa Yesu (Yohana 15:8)Sasa basi ,ni muhimu kufahamu
kwamba upendo ni tunda la Roho,tunalolipokea kutoka kwa Roho Mtakatifu.Tukilipokea tunda hili,na kukua
kila siku katika upendo (1Wathesalonike 3:12),Kama matunda yanavyokua,ndipo tunapokuwa wanafunzi wa Yesu kwelikweli.Tukiwa na tunda la Roho la upendo,tunakuwa na Furaha ya wokovu ambayo haiwezi kuondoka kwetu kwa sababu ya majaribu yoyote au kukosekana kwa lolote la kimwili(Yakobo1:2).
Tutakuwa na amani ipitayo fahamu zote(Wafilipi 4:7)inayotuwezesha kuwa na amani na watu ambao tusingeweza kuwa na amani nao.Tutakuwa na lengo la kutafuta amani na watu wote wakati wote(Waebrania 12:14)Tutakuwa na uvumilivu wa kipekee katika mateso,makwazo kutoka kwa watu n.k Tutakuwa na utu wema kwa watu wengine hata wale ambao hawajaokoka
(Marko 10:17).Tutakuwa na fadhili yaani hali ya kutaka wakati wote watu wanaotuzunguka wawe na furaha.
Tutakuwa watu tuliojaa imani,tusiotetereka kirahisi.Tutakuwana upole yaani unyenyekevu (Mathayo 11:29;
Wafilipi2:5-8)Na pili tutakuwa na kiasi (self-control)yaani uwezo wa kukataa kufanya lile ambalo Yesu hataki, kwa gharama yoyote.Je,unataka kuwa na tunda la Roho katika maisha yako?Mwambie Roho Mtakatifu,naye atafanya.
3:ROHO MTAKATIFU,ROHO ATUSAIDIAYE KUOMBA
Kila Mkristo,au mtu aliyeokoka,hana budi kuwa na lengo la kufikia kimo na cheo cha utimilifu wa Kristo katika tabia na Utumishi wa
Mungu(Waefeso 4:11-15)Kufikia kiwango cha Yesu Kristo katika tabia ni jambo linalowezekana,Kama siyo,tusingetakiwa
kuwa wakamilifu na watakatifu kama Baba wa mbinguni alivyo Mtakatifu(Mathayo 5:48;1`Petro 1:15-16)Neno la Mungu pia,
linatufundisha uwezekano wa kuwa na viwango vya utumishi vya yesu alipokuwa duniani,na hata kuzidi(Yohana 14:12).Hata
hivyo haya yote hayawezekani kama sisi siyo waombaji kama Yesu alikuwa mwombaji namba moja.Alifanya maombi alfajiri na mapema
(Marko 1:35).Alijitenga na shughuli mchana na kufanya maombi (Luka 5:15-16)Aliomba jioni (Mathayo 14:23)Wakati mwingine
alifanya maombi usiku kucha(Luka 6:12)Je,sisi tunaweza kuwa waombaji kiasi hiki?Kwa nguvu na jitihada zetu hatuwezi.
Tunaweza tu,tukisaidiwa na Roho Mtakatifu.Ndiyo maana tunajifunza somo hili muhimu leo katika mfululizo wa masomo haya
ya Roho Mtakatifu ,na kichwa cha somo la sasa ni ” ROHO MTAKATIFU,ATUSAIDIAYE KUOMBA”,
NA TUTAJIFUNZA SOMO HILI KATIKA VIPENGERE VINNE:-
6. UMUHIMU WA MAOMBI KATIKA MAISHA YA KIROHO
7. KUSHUKA KWA MUNGU BAADA YA MAOMBI YA KUUGUA NA KULIA
8. MAFUNDISHO TUNAYOYAPATA KUTOKANA NA MAOMBI YA YESU
9. ROHO MTAKATIFU,MSAIDIZI ATUSAIDIAYE KUOMBA
2. UMUHIMU WA MAOMBI KATIKA MAISHA YA KIROHO
Shetani ndiye adui yetu mkuu.Kazi yake ni kuiba chochote kizuri cha kiroho tulicho nacho,na tena kuchinja au kuua na kuharibu yote
mema kwetu kiroho na kimwili.Tukiwa peke yetu,kamwe hatuwezi kupambana na shetani na kumshinda.Hatuna budi kuwa na
Mungu katika maisha yetu ili tumshinde ibilisi.Daudi alimshinda Goliathi kwa Jina la Bwana.Hakumshinda kwa nguvu zake.Kwa maana nyingine hatuwezi kuzaa matunda yoyote mema ya kiroho kama hatuko ndani ya Yesu.Usalama wetu na ushindi wetu wa kiroho,unategemeana
sana na sisis kukaa ndani yake Yesu,yaani sisi kuwa na uhusiano au ushirika na Kristo.Pasipo yeye,sisi hatuwezi kufanya neno lolote
.(Yohana 15:4-5).Kukaa ndani ya Yesu,kunafananishwa na tawi lililounganishwa na shina.Kuunganishwa huko ndiyo uhai wa tawi.
Tawi likijitenga na shina,linanyauka na kufa.Sasa basi,tunaunganisha na Mungu na Mungu tunapokuwa tunawasiliana naye katika maombi.Tukiwa hatuna maisha ya maombi,kimsingi ni kwamba tunakuwa ni tawi lililojenga na shina,na hivyo tunanyauka na hatimaye
kufa kiroho.Hatuwezi kuwa na kitu tusipoomba(Yakobo 4:2)
Tutaingia majaribuni tusipoomba (Mathayo 26:41).Tutapepetwa kama ngano na ibilisi na mazuri yote ya kiroho yataondoshwa,na
imani yetu itatoweka(Luka 22:31-32).Shetani atatumeza na kuturudisha katika ufalme wake(1Petro 5:8).Hatuwezi kuwaleta watu
kwa Yesu,tusipokuwa waombaji,maana Shetani hatawaachia(Zaburi 2:8).Hatuwezi kuona watu wakifunguliwa katika vifungo vya
shetani vya kimwili(Luka 13:16) na vile vinavyotokana na mambo ya rohoni (Matendo 12:5-17).Kwa ufupi tutachukuliwa na
mafuriko ya Shetani(Zaburi 32:6).
3. KUSHUKA KWA MUNGU BAADA YA MAOMBI YA KUUGUA NA KULIA
Maandiko yanatufahamisha kwamba makao ya Mungu mbinguni,ni Mahali palipoinuka,na Mlimani kwenye kiti cha enzi
cha Mungu (Isaya 57:15;Kutoka 24:12-13;Ufunuo 7:9-10).Ingawa Mungu wetu yuko mlimani,maandiko yanasema
tukimwomba,yeye husikia huko mbinguni na kutujibu maombi yetu kwa kuyatenda tunayoyataka (1Wafalme 8:32;Zaburi 76:8;102:19).Hata hivyo,hatuna budi kufahamu pia kwamba katika mazingira Fulani Mungu hushuka kutoka mlimani na kuja
duniani katika hali isiyo ya kawaida.Mungu anaposhuka kwa jinsi hii,hutenda mambo ya kutisha,na ya kushangaza,yasiyo ya
kawaida na hivyo kuwavuta wengi mno kwake(Waamuzi 4:12-16,5:13;Isaya 31:4;Hesabu 11:23-25,31-32).Uamsho hutokea
Mungu anaposhuka,na watu wagumu wa mioyo huvutwa kwa Yesu,walio vuguvugu huwa moto,mambo mengine makubwa ya
kuitikisa jamii kama mamia ya wenye ukimwi kupona kwa mpigo,hutokea,Mungu akishuka.
Hata hivyo kushuka kwa Mungu hutokea baada ya maombi ya kuugua na kulia kwa uchungu mkubwa(Kutoka 2:23-24;3:7-8;
Matendo 7:32-34).Wakati wote Yesu Kristo alimfanya Mungu kushuka katika huduma yake kwa kuwa aliomba kwa kulia sana
na machozi(Waebrania 5:7),na wengine walimuombolezea kwa kilio na uchungu mkubwa(Luka 23:27)Kulia kwa kuugua katika
maombi hushusha majibu ya maombi namna ya kipekee(2Nyakati 34:27;Zaburi 34:17;39:12;51:1-2,17;72:12;12;88:1-2;Isaya 58:9;Yeremia 31:9;Luka 18:7).Sasa basi ni rahisi kuomba maombi kwa kulia na kuugua?jibu ni la,bila msaada wa Roho Mtakatifu,itakuwa kama tunaigiza tu.
4. MAFUNDISHO TUNAYOYAPATA KUTOKANA NA MAOMBI YA YESU
Tunajifunza mambo mengi zaidi kuhusiana na maombi kwa kuyaangalia maisha ya maombi ya Yesu,na
mafundisho yake kuhusu maombi:-
§ Yesu Kristo alikuwa na wakati wa kuomba pamoja na wanafunzi wake(Luka 9:18),Lakini pia alikuwa na muda mrefu wa
maombi ya peke yake (Luka 5:16;Marko 6:45-46).Ni muhimu kujiunga na kikosi cha maombi cha Kanisa na kushiriki
maombi
ya pamoja na wengine,lakini ni lazima kila mmoja kuwa na muda wa kuomba mwenyewe.
§ Yesu hakukubali kuchukuliwa na huduma za kushauri watu,kuwaombea watu n.k na kuziruhusu zimkoseshe kuomba.
Alijua bila maombi,huduma hizo zitakuwa hazina nguvu.Aliziacha huduma,akafanya maombi(Luka 5:15-16).Kabla ya
kuzungumza na watu,alizungumza na Mungu KWANZA.Alifanya maombi ya alfajiri na mapema sana na baadaye
alipokutana na watu ilikuwa rahisi mno kwake kuponya ukoma na kutoa pepo.(Marko 1:35-42).
§ Kabla ya Yesu kutembea juu ya maji,na kukomesha upepo,alikuwa na kipindi kirefu cha maombi(Marko 6:46-51).Vipindi virefu vya maombi vinaweza kutupa uwezo wa kuona yasiyowezekana yakiwezekana!
§ Utukufu wa Yesu ulitokana na maombi!(Luka 9:28-29)Hatuna utukufu wa Mungu kwa kuwa siyo waombaji!Mwombaji,
utukufu wake humwogopesha shetani
§ Alipokuwa na huzuni aliomba hakunung’unika tu na kulalamika,na ghafla alipata ujasiri wa kukabili lolote lile
(Mathayo 26:36-39;47-49).Hatuna ujasiri na tumejaa woga kwa kuwa hatuombi
§ Maombi yake yalikuwa ni vita hasa.Alipokuwa akiomba,alitoka jasho(hari)kama matone ya damu(Luka 22:44)
.Maombi ni mapambano dhidi ya shetani anayezuia majibu yetu(Danieli 10:12-13).Ni lazima iwe ni vita.Mwili ni lazima
tuushughulishe kama wapiganaji hasa,tukiwa katika roho Maombi yenye matokeo makubwa,ni yale ya kutoka jasho!Ni
lazima tumkabili shetani katika vita ya maombi kabla hata hajatushambulia.Katika vita ya siku sita kati ya waisraeli na wamisri,
miaka kadha iliyopita;Waisraeli walishinda Wamisri ingawa walikuwa na ndege nyingi zaidi za kivita kuliko wao,kwa kuwa
walizipiga KABLA hazijaondoka katika vituo vyao.Tusingoje matatizo ndio tuombe!
§ Imani yetu na ya ndugu zetu,inaweza kutokutindika,ikiwa tu tutakuwa waombaji;kinyume cha hapo ni rahisi kumezwa na
shetani(Luka 22:31-32;1Petro 5:8-9)
§ Maombi ndiyo yanafanya tuutunze utakatifu wetu,na kuwa mbali na dunia.Bila maombi ni rahisi kuvutwa na masumbufu
ya dunia(Luka 21:34-36)
§ Yesu aliliombea Kanisa(Yohana 17:14-15).Ni muhimu kuliombea kanisa na siyo kujiombea wenyewe tu wakati wote.
Je tunaweza kuyatendea kazi yote haya kwa nguvu zetu?jibu ni la.Kwa nguvu zetu hatuwezi,bila msaada wa Roho Mtakatifu.
5. ROHO MTAKATIFU MSAIDIZI ATUSAIDIAYE KUOMBA
Shetani anafahamu sana umuhimu wa maombi,na hivyo atatuzuia sana kufanya maombi kuliko yote mengine,
ili tubaki kama matawi ambayo hayajaunganishwa na shina.Anajua pasipo Mungu,sisi hatuwezi neon lolote.
Kwa kujifunza tu juu ya maombi,bado hatuwezi kuwa na maisha ya maombi.Tunaweza kuomba sisi hatuwezi
neon lolote.Kwa kujifunza tu juu ya maombi,bado hatuwezi kuwa na maisha ya maombi.Tunaweza kuomba
siku mbili,tatu,halafu basi.Pamoja na wanafunzi wa Yesu kuhimizwa kuomba na Yesu mwenyewe,bado
walishindwa kuwa waombaji(Matahyo 26:37-43).Ndipo hatimaye akawaambia atakuja Msaidizi ambaye
kazi yake mojawapo,ni kutusaidia kuomba(Yohana 16:7;Warumi 8:26-28).Yeye Roho,kwa kuwa
hutuombea kwa kuugua,na tena ni Roho ya neema na kuomba,huweza kutupa msaada wa kutuwezesha
kuomba kwa kuugua na kulia(Zekaria 12:10)Baada ya Roho Mtakatifu kuja na kuwasaidia wanafunzi wa
Yesu,maisha yao ya maombi yalibadilika(Matendo 10:9).Siri ni hii,usitumie nguvu zako kuomba.Kabla ya
kuingia katika maombi,mwombe Msaidizi akusaidie kuomba.
UBATIZO WA ROHO MTAKATIFU
Ili tuweze kuwa mashahidi wa Mungu,tunahitajika kubatizwa kwa Roho Mtakatifu baada ya kuokoka na kutakaswa.Ili tumtendee Mungu
kazi kikamilifu,ni lazima tupokee nguvu ya Roho Mtakatifu (Matendo 1:8;Luka 24:49).Kwa sababu hili,somo hili,ni la muhimu sana
kwa mtu yeyote anayetaka kuwa mtendakazi mzuri wa Mungu.Tutaligawa somo hili katika vipengere vinne:-
10. MAANA YA UBATIZO WA ROHO MTAKATIFU
11. UBATIZO WA ROHO MTAKATIFU,UWEZA WA KUTUWEZESHA KUWA MASHAHIDI WA MUNGU
12. ALAMA 9 ZA ROHO MTAKATIFU NA JINSI ZINAVYOTUPAUFAHAMU KUHUSU
UBATIZO WA ROHO MTAKATIFU
13. JINSI YA KUBATIZWA KWA ROHO MTAKATIFU
14. ISHARA YA KWANZA YA KUBATIZWA KWA ROHO MTAKATIFU NA NIDHAMU INAYOAMBATANA
15. UMUHIMU WA KUUCHOCHEA MOTO WA ROHO MTAKATIFU
Subscribe to:
Posts (Atom)