Soma kwa Kumbukumbu Zako Maneno haya Ya Lowassa.
"Mheshimiwa Spika, kwanza napenda kuchukua nafasi hii kukushukuru sana kwa kunifanya msemaji wa kwanza katika hoja hii.
Lakini la pili, nimpongeze Dk. Harrison Mwakyembe, Mwenyekiti wa Kamati
Teule kwa kuwasilisha kwa mbwembwe nyingi sana taarifa yake, mbwembwe
zilikuwa nzuri kweli.
Kwa kazi nzuri kwa maoni yao,
wamewasilisha vizuri. Lakini nimesimama kuweka kwenye kumbukumbu
kutoridhika kwangu na jinsi kazi hiyo ilivyofanywa.
Mheshimiwa
Dk. Harrison Mwakyembe ni mwanasheria, alikuwa anafundisha wanafunzi
Chuo Kikuu. Moja ya vitu alivyokuwa anafundisha ni 'NATURAL JUSTICE'.
Mheshimiwa Spika, wewe pia ni mwanasheria unafahamu suala la 'NATURAL
JUSTICE'. Kwamba Kamati Teule imesikiliza watu wengine wote pamoja na
wanaoita minong'ono ya mitaani. Wamesafiri mpaka Marekani kutafuta
mashahidi, lakini mimi ambaye ni mmoja katika watuhumiwa mle
hawakunihoji hata siku moja.
Mheshimiwa Spika, nimesimama
kueleza masikitiko yangu. Ofisi ya Bunge mpaka ofisini kwangu (Dar es
Salaam) hata wangeniita ningekwenda kwa miguu kama hamna gari na
nilikuwa tayari kufanya hivyo.
Hawa ni watu makini sana siwezi
kuamini kwamba wanaweza wakafanya 'oversight' kama hiyo. Kwa sababu
katika kila hoja walizojenga wamesema 'Waziri Mkuu ilikuwa hivi'.
Kulikuwa na shida gani kuja kuniuliza 'Waziri Mkuu wanasema ulitoa
dokezo hili ni sawa sawa ni kweli'? Kulikuwa na shida gani kwa mfano
kufuata utaratibu wa Westmister kuthibitisha hapo unaposema mwenye
Richmond ni fulani uka-lay on the table records na ushahidi kuwa ni
fulani.
Mheshimiwa Spika, Taifa letu ni Taifa changa, lakini
chombo hiki ndiyo mahali pa demokrasia pakubwa katika nchi pote, hapa
ndipo penyewe.
Kama katika chombo hiki hakitaonekana kutendeka
haki nchi yetu haitakwenda vizuri. Hapa ndipo tunategemea tuwaonyeshe
umakini wetu, umahiri wetu katika mambo ya demokrasia.
Kwa
hiyo, nilichofanyiwa napenda kuweka kumbukumbu sawa kwamba, naona si
sahihi, NIMEFADHAIKA SANA, NIMEDHALILISHWA SANA, NIMEONEWA SANA KATIKA
HILI.
Maana zimechukuliwa tuhuma zikaja zikaelezwa hapa kwamba
hivi ndivyo ilivyo. Mimi sijaulizwa. Kulikuwa na shida gani ya
kuniuliza, kwa nini muamini minong'ono ya mitaani kuliko maelezo zangu?
SISI WOTE HAPA NI WANASIASA, TUKIANZA KUAMINI MINONG'ONO YA MITAANI
NIAMBIENI MWANASIASA ATAKAYESIMAMA. Hatuwezi, Tume imepewa muda wa
kutosha lakini inashindwa kumuona mtu ambaye wanamtuhumu na wanamsema
kwa kirefu sana.
Mheshimiwa Spika, lakini hata pale uliponinong'oneza ukaniambia una ushahidi wowote? Nilikuwa na ushahidi huo wa maandishi.
Katika taarifa yao hakuna hata moja ya ushahidi ambao umetoka kwa
Waziri Mkuu. Kile kitabu cha majedwali kimejaa majedwali mengi pamoja na
magazeti mpaka ya udaku lakini maelezo ya Waziri Mkuu hakuna hata moja.
Mheshimiwa Spika naamini ingekuwa ni heshima kubwa wangeiweka halafu
wakasema tunakataa kitambulisho hiki kwa sababu hii na hii, hiyo ndiyo
imejengwa hoja.
Lakini kujenga hoja na kuja hapa bungeni
tunahutubia nchi nzima na kusema Waziri Mkuu amefanya hiki, amefanya
hiki bila ya kumsikiliza nachelea kuuliza hivi mtu wa chini itakuwaje?
Mheshimiwa Spika, lakini nimetafakari kwa makini sana jambo hili
nikajiuliza hivi hasa kulikoni mpaka watu wazima, wenye uwezo wao, watu
maarufu wenye heshima zao, mpaka wafike mahali waache jambo la msingi
kama hilo, kulikoni?
Mimi nadhani there is a wish which I am
going to grant, ni Uwaziri Mkuu. Kwamba ionekane Waziri Mkuu ndio
amefanya haya, tumuondolee heshima au tumwajibishe.
Mheshimiwa
Spika, nimetafakari sana kwa NIABA YA CHAMA CHANGU, KWA NIABA YA
SERIKALI YANGU nimeamua kumwandikia Rais barua ya kumwomba niachie
ngazi.
Nafanya hivyo kwa moyo mweupe kabisa ili kuonyesha DHANA
YA UWAJIBIKAJI lakini na KUTOKUBALIANA NA UTARATIBU ULIOTUMIKA KUSEMA
UONGO NDANI YA BUNGE WA KUMSINGIZIA MTU.
Edward Lowassa (MP),
Rtd PM..
Think Twice..
"Mheshimiwa Spika, kwanza napenda kuchukua nafasi hii kukushukuru sana kwa kunifanya msemaji wa kwanza katika hoja hii.
Lakini la pili, nimpongeze Dk. Harrison Mwakyembe, Mwenyekiti wa Kamati
Teule kwa kuwasilisha kwa mbwembwe nyingi sana taarifa yake, mbwembwe
zilikuwa nzuri kweli.
Kwa kazi nzuri kwa maoni yao, wamewasilisha vizuri. Lakini nimesimama kuweka kwenye kumbukumbu kutoridhika kwangu na jinsi kazi hiyo ilivyofanywa.
Mheshimiwa Dk. Harrison Mwakyembe ni mwanasheria, alikuwa anafundisha wanafunzi Chuo Kikuu. Moja ya vitu alivyokuwa anafundisha ni 'NATURAL JUSTICE'.
Mheshimiwa Spika, wewe pia ni mwanasheria unafahamu suala la 'NATURAL JUSTICE'. Kwamba Kamati Teule imesikiliza watu wengine wote pamoja na wanaoita minong'ono ya mitaani. Wamesafiri mpaka Marekani kutafuta mashahidi, lakini mimi ambaye ni mmoja katika watuhumiwa mle hawakunihoji hata siku moja.
Mheshimiwa Spika, nimesimama kueleza masikitiko yangu. Ofisi ya Bunge mpaka ofisini kwangu (Dar es Salaam) hata wangeniita ningekwenda kwa miguu kama hamna gari na nilikuwa tayari kufanya hivyo.
Hawa ni watu makini sana siwezi kuamini kwamba wanaweza wakafanya 'oversight' kama hiyo. Kwa sababu katika kila hoja walizojenga wamesema 'Waziri Mkuu ilikuwa hivi'. Kulikuwa na shida gani kuja kuniuliza 'Waziri Mkuu wanasema ulitoa dokezo hili ni sawa sawa ni kweli'? Kulikuwa na shida gani kwa mfano kufuata utaratibu wa Westmister kuthibitisha hapo unaposema mwenye Richmond ni fulani uka-lay on the table records na ushahidi kuwa ni fulani.
Mheshimiwa Spika, Taifa letu ni Taifa changa, lakini chombo hiki ndiyo mahali pa demokrasia pakubwa katika nchi pote, hapa ndipo penyewe.
Kama katika chombo hiki hakitaonekana kutendeka haki nchi yetu haitakwenda vizuri. Hapa ndipo tunategemea tuwaonyeshe umakini wetu, umahiri wetu katika mambo ya demokrasia.
Kwa hiyo, nilichofanyiwa napenda kuweka kumbukumbu sawa kwamba, naona si sahihi, NIMEFADHAIKA SANA, NIMEDHALILISHWA SANA, NIMEONEWA SANA KATIKA HILI.
Maana zimechukuliwa tuhuma zikaja zikaelezwa hapa kwamba hivi ndivyo ilivyo. Mimi sijaulizwa. Kulikuwa na shida gani ya kuniuliza, kwa nini muamini minong'ono ya mitaani kuliko maelezo zangu?
SISI WOTE HAPA NI WANASIASA, TUKIANZA KUAMINI MINONG'ONO YA MITAANI NIAMBIENI MWANASIASA ATAKAYESIMAMA. Hatuwezi, Tume imepewa muda wa kutosha lakini inashindwa kumuona mtu ambaye wanamtuhumu na wanamsema kwa kirefu sana.
Mheshimiwa Spika, lakini hata pale uliponinong'oneza ukaniambia una ushahidi wowote? Nilikuwa na ushahidi huo wa maandishi.
Katika taarifa yao hakuna hata moja ya ushahidi ambao umetoka kwa Waziri Mkuu. Kile kitabu cha majedwali kimejaa majedwali mengi pamoja na magazeti mpaka ya udaku lakini maelezo ya Waziri Mkuu hakuna hata moja.
Mheshimiwa Spika naamini ingekuwa ni heshima kubwa wangeiweka halafu wakasema tunakataa kitambulisho hiki kwa sababu hii na hii, hiyo ndiyo imejengwa hoja.
Lakini kujenga hoja na kuja hapa bungeni tunahutubia nchi nzima na kusema Waziri Mkuu amefanya hiki, amefanya hiki bila ya kumsikiliza nachelea kuuliza hivi mtu wa chini itakuwaje?
Mheshimiwa Spika, lakini nimetafakari kwa makini sana jambo hili nikajiuliza hivi hasa kulikoni mpaka watu wazima, wenye uwezo wao, watu maarufu wenye heshima zao, mpaka wafike mahali waache jambo la msingi kama hilo, kulikoni?
Mimi nadhani there is a wish which I am going to grant, ni Uwaziri Mkuu. Kwamba ionekane Waziri Mkuu ndio amefanya haya, tumuondolee heshima au tumwajibishe.
Mheshimiwa Spika, nimetafakari sana kwa NIABA YA CHAMA CHANGU, KWA NIABA YA SERIKALI YANGU nimeamua kumwandikia Rais barua ya kumwomba niachie ngazi.
Nafanya hivyo kwa moyo mweupe kabisa ili kuonyesha DHANA YA UWAJIBIKAJI lakini na KUTOKUBALIANA NA UTARATIBU ULIOTUMIKA KUSEMA UONGO NDANI YA BUNGE WA KUMSINGIZIA MTU.