SIRI YA MAOMBI YANAYOJIBIWA.
Anatoli Levitini, mwandishi na
mwanahistoria wa Kirusi, alitumia miaka yake mingi katika Gulag ya Siberia,
ambako dua zilizotolewa kwa Mungu zilionekana kana kwamba zimeganda ardhini.
Lakini alirudi akiwa mzima kiroho. "Mwujiza mkuu kuliko yote ni
maombi," aliandika. "Yanipasa tu kumgeukia Mungu kimawazo na mara
moja naisikia nguvu inayoingia ndani yangu kutoka mahali fulani, inaingia
katika roho yangu, na mwili wangu wote. Je! hicho ni kitu gani? Je, naweza
kuipata wapi hiyo nguvu inifanyayo mimi kuwa mtu mpya na kuniokoa mimi, niliye
mzee duni sana, niliyechoka na maisha, ambayo itaniinua juu ya dunia hii?
Inatoka nje yangu - wala hakuna nguvu yo yote ulimwenguni humu ambyo ingeweza
kuipinga."
Katika mwongozo huu tunaona
jinsi maombi yanavyotusaidia kujenga uhusiano wenye nguvu zaidi pamoja na
maisha ya Kikristo yenye nguvu.
1. Kuzungumza Na Mungu
Je, tunawezaje kuwa na uhakika
kwamba Mungu anatusikia tunapoomba?
"Ndipo mtaniita mimi na kwenda KUNIOMBA, nami NITA SIKILIZA. Nanyi mtanitafuta na kuniona, mtakaponitafuta kwa moyo wenu wote." - Yeremia 29:12,13.
"Ndipo mtaniita mimi na kwenda KUNIOMBA, nami NITA SIKILIZA. Nanyi mtanitafuta na kuniona, mtakaponitafuta kwa moyo wenu wote." - Yeremia 29:12,13.
Je, ni uthibitisho gani aliotoa
Yesu kuonyesha kwamba atasikia na kujibu maombi yetu?
"Basi nawaambia, Ombeni, nanyi mtapewa; tafuteni, nanyi mtaona; bisheni, na mlango utafunguliwa kwenu." - Luka 11:9.
"Basi nawaambia, Ombeni, nanyi mtapewa; tafuteni, nanyi mtaona; bisheni, na mlango utafunguliwa kwenu." - Luka 11:9.
Maombi ni maongezi ya pande
mbili. Hii ndiyo maana Yesu anaahidi anasema:
"Tazama nasimama mlangoni, nabisha. Mtu ye yote akiisikia sauti yangu, na kuufungua malngo, nitaingia na kula pamoja naye, na yeye pamoja nami." - Ufunuo 3:20.
"Tazama nasimama mlangoni, nabisha. Mtu ye yote akiisikia sauti yangu, na kuufungua malngo, nitaingia na kula pamoja naye, na yeye pamoja nami." - Ufunuo 3:20.
Kwa jinsi gani inawezekana kwetu
kuketi na kuwa na maongezi mazuri wakati wa chakula cha jioni pamoja na Kristo?
Kwanza, kwa kumwambia kila kitu tulicho nacho moyoni mwetu kwa njia ya maombi.
Pili, kwa kusikiliza kwa makini. Tunapotafakari wakati wa maombi, Mungu anaweza
kuongea nasi moja kwa moja. Na tunapolisoma Neno la Mungu kwa roho ya ibada,
Mungu ataweza kuongea nasi kupitia katika kurasa zake.
Maombi yanaweza kuwa njia ya
maisha kwa Mkristo.
"OMBENI
BILA KUKOMA; shukuruni kwa kila jambo, maana hayo ndiyo mapenzi ya Mungu kwenu
katika Kristo Yesu." - 1 Wathesalonike 5:16-18.
Je! sisi tunawezaje "kuomba
bila kukoma?" Je, yatupasa kupiga magoti wakati wote au kurudia-rudia
kusema maneno ya kumsifu au kutoa dua? La, hasha. Lakini tunapaswa kuishi
karibu sana na Yesu kiasi cha kujisikia huru kusema naye wakati wo wote, na
mahali po pote.
"Tukiwa katika makundi ya
watu mitaani, katika shughuli ya kibiashara, tunaweza kutoa dua yetu kwa Mungu
na kumsihi atupe uongozi wake… Daima tungeacha wazi mlango wa moyo wetu na
kuuacha mwaliko wetu ukipanda juu ili Yesu aweze kuja moyoni mwetu na kukaa
humo kama mgeni wetu wa mbinguni." - Steps to Christ, uk. 99.
Mojawapo ya njia bora sana ili
kujenga uhusiano huo wa karibu sana ni kujifunza kutafakari wakati tunapoomba.
"Kutafakari
kwangu na kumpendeze yeye, mimi ninapomfurahia BWANA." -Zaburi 104:34.
Unapoomba usiharakishe tu
kupitia orodha ya mambo unayotaka. Ngojea. Sikiliza. Kutafakari kidogo ukiwa
katika maombi kunaweza kuuboresha sana uhusiano wako na Mungu.
"Mkaribieni
Mungu, naye atawakaribia ninyi." - Yakobo 4:8.
Kadri sisi tunavyozidi
kumkaribia sana Yesu ndivyo kadri tunavyoweza kuonja kuwako kwake. Basi wewe
unapaswa kuwa katika umbali wa kuweza kuongea na Yesu, wala usiwe na wasi wasi
juu ya kusema maneno yaliyo sahihi. Ongea tu naye kwa unyofu wa moyo na bila
kuficha kitu. Ongea juu ya kila kitu. Yeye amepitia maumivu makali sana ya kifo
kile chenyewe ili apate kuwa Msiri wako.
2. Jinsi Ya Kuomba
Tunapoingia katika maombi,
tunaweza kupenda kufuata muhtasari wa sala ya Bwana, sala ya mfano ambayo Yesu
aliwafundisha wanafunzi wake kuitikia ombi lao hili:
Tufundishe sisi kuomba.
"Baba yetu uliye mbinguni, jina lako litukuzwe, ufalme wako uje, mapenzi yako yatimizwe hapa duniani kama huko mbinguni. Utupe leo riziki yetu. Utusamehe deni zetu, kama sisi nasi tulivyowasamehe wadeni wetu. Wala usitutie majaribuni, lakini utuokoe na yule mwovu, kwa kuwa ufalme ni wako, na nguvu, na utukufu, hata milele. Amina" - (Mathayo 6:9-13).

Kulingana na mfano huo ambao Yesu
aliutoa katika sala yake, sisi tunatakiwa kumwendea Mungu kama Baba yetu aliye
mbinguni. Tumwombe kwamba mapenzi yake yatawale mioyo yetu kama vile mapenzi
yake yanavyotawala katika mbingu yote. Tunamtafuta ili atupatie mahitaji yetu
ya kimwili, msamaha wake, kwa ajili ya kuwa na roho ya kuwasamehe wengine.
Kumbukeni ya kwamba uwezo wetu
wa kuipinga dhambi unatoka kwa Mungu. Sala ya Kristo inahitimisha kwa maneno ya
sifa kwake.
Safari nyingine Yesu
aliwafundisha wanafunzi wake kumwomba Baba "kwa jina langu" (Yohana
16:23) - yaani, kuomba kulingana na kanuni zake Yesu. Hii ndiyo maana Wakristo
kwa kawaida hufunga sala zao kwa maneno haya: "Katika jina la Yesu,
Amina." Amen (amina) ni neno la Kiebrania limaanishalo "Na iwe hivyo".
Japokuwa sala ya Bwana inatoa
mwongozo juu ya mambo tunayotakiwa kuyaomba na jinsi ya kutunga sala,
mawasiliano yetu na Mungu yanakuwa bora sana kama yanatoka moyoni mwetu kwa
hiari.
Tunaweza kuomba juu ya kila
kitu. Mungu anataka tumwombe msamaha kwa dhambi zetu (1Yohana 1:9), tumwombe
atuongezee imani (Marko 9:24), tumwombe uponyaji wa maumivu na magonjwa yetu
(Yakobo 5:15), na kumwagiwa kwa Roho (Zakaria 10:1). Yesu anatuthibitishia
kwamba tunaweza kumpelekea yeye mahitaji yetu yote, pamoja na mashaka yetu; mno
kuweza kumwomba.
("Mwekeeni
matatizo yenu yote, maana yeye anawatunzeni") - 1 Petro 5:7.
Mwokozi wetu anapendezwa na
mambo yo yote madogo yahusuyo maisha yetu. Moyo wake huchangamka wakati
inapomwendea mioyo yetu kwa upendo na imani.
3. Maombi Ya Faragha
Wengi wetu tunayo mambo fulani
ambayo tunasita kuwaambia hata marafiki zetu wa karibu sana. Kwa hiyo, Mungu
anatualika sisi kuutua mzigo huo katika maombi yetu ya faragha: tukiwa kila
mmoja peke yake na yeye. Si kwamba yeye anahitaji maelezo yote. Mwenyezi anajua
vizuri sana kuliko sisi tunavyojua, makusudi yetu yaliyojificha moyoni mwetu,
na chuki zetu zilizojificha ndani. Lakini tunahitaji kuifunua mioyo yetu kwake
yeye atujuaye mpaka ndani kabisa, na atupendaye milele. Uponyaji unaweza kuanza
Yesu anapoweza kuyagusa majeraha yetu.
Tuombapo, Yesu, Kuhani wetu
Mkuu, yu karibu nasi kutusaidia:
"Tunaye mmoja ALIYEJARIBIWA KWA KILA NJIA, KAMA SISI TUNAVYOJARIBIWA -lakini alikuwa hana dhambi. Basi na tukikaribie kiti cha neema kwa ujasiri, ili tupate kupokea rehema na kupata neema ya kutusaidia wakati wa mahitaji" - (Waebrania 4:15,16).

Je, una wasi wasi, mfadhaiko,
hatia? Weka hayo mbele zake Bwana. Ndipo yeye anaweza kukidhi kila hitaji
tulilo nalo. Je, ni lazima tuwe na mahali maalumu pa maombi hayo ya faragha?
"wewe unaposali, ingia katika chumba chako, funga mlango na kumwomba Baba yako, ambaye.. atakujazi." - Mathayo 6:6.
"wewe unaposali, ingia katika chumba chako, funga mlango na kumwomba Baba yako, ambaye.. atakujazi." - Mathayo 6:6.
Zaidi ya kuomba wakati wa
kutembea mitaani, kufanya kazi, au kufurahia mkutano fulani, kila Mkristo
angekuwa na muda fulani uliotengwa kila siku kwa maombi yake yeye peke yake
pamoja na kujifunza Biblia. Tunza miadi yako ya kila siku na Mungu wako wakati
unapokuwa mchangamfu sana na wakati unapokuwa makini sana.
4. Maombi Ya Hadhara
Kujiunga pamoja na wengine
katika maombi huwaunganisha watu kwa kifungo maalum na kukaribisha uweza wa
Mungu kwa njia ya pekee.
"Kwa
kuwa wawili au watatu wanapokusanyika pamoja katika jina langu, nipo pamoja nao
pale." - Mathayo 18:20.
Mojawapo ya mambo makuu kuliko
yote tuwezayo kufanya sisi kama familia ni kukuza maisha ya maombi ya pamoja.
Waonyesheni watoto kwamba tunaweza kupeleka mahitaji yetu kwake moja kwa moja.
Watakuwa na msisimko juu ya Mungu watakapoona anajibu maombi yanayohusu mambo
halisi ya maisha yao. Ifanyeni ibada ya familia kuwa wakati wa furaha na
kubadilishana uzoefu wa maisha katika hali ya uhuru.
5. Siri Saba Za Maombi
Yanayojibiwa
Musa alipoomba, Bahari ya Shamu
iligawanyika. Eliya alipoomba, moto ulishuka kutoka mbinguni. Danieli
alipoomba, malaika aliyafumba makanwa ya simba wale wenye njaa kali. Biblia
inatueleza visa vingi vya kusisimua vya maombi yaliyojibiwa. Tena inapendekeza
kwetu maombi kama njia ya kupata ule uweza kwetu maombi kama njia ya kupata ule
uweza mkuu wa Mungu. Yesu anaahidi hivi:
"Mkiniomba neno lo lote kwa jina langu, nami nitalifanya" - (Yohana 14:14).
"Mkiniomba neno lo lote kwa jina langu, nami nitalifanya" - (Yohana 14:14).
Lakini maombi mengine bado
yanaonekana kana kwamba hayasikilizwi. Kwa nini? Hapa chini zipo kanuni saba
zitakazokusaidia wewe kuomba kwa ufanisi zaidi:
(1) Uwe karibu sana na Kristo.
"NINYI MKIKAA NDANI YANGU, na maneno yangu yakikaa ndani yenu, ombeni mtakalo lote nanyi mtapewa." - Yohana 15:7.
"NINYI MKIKAA NDANI YANGU, na maneno yangu yakikaa ndani yenu, ombeni mtakalo lote nanyi mtapewa." - Yohana 15:7.
Tunapoupa kipaumbele uhusiano
wetu na Mungu na kuwa karibu naye, tutakuwa tunasikiliza na kutazamia kupata
majibu kwa maombi yetu ambayo, vinginevyo, tusingeyatambua.
(2) Endelea Kumtumaini Mungu.
"MKIAMINI, mtapokea yote myaombayo katika sala zenu" - (Mathayo 21:22).
"MKIAMINI, mtapokea yote myaombayo katika sala zenu" - (Mathayo 21:22).
Kuamini au kuwa na imani, maana
yake ni kwamba tunamtazamia Baba yetu aliye mbinguni kwamba kweli atatupa hayo
mahitaji yetu. Kama wewe una wasiwasi kwamba huna imani, basi, kumbuka kwamba
Mwokozi alitenda mwujiza kwa mtu yule aliyemsihi sana akiwa amekata tamaa,
aliyesema:"
"Naamini, nisaidie kutokuamini kwangu!" - (Marko 9:24).
"Naamini, nisaidie kutokuamini kwangu!" - (Marko 9:24).
Wewe kazana tu kuitumia imani
ULIYO nayo; usiwe na waiswasi juu ya imani ile usiyo nayo.
(3) Jisalimishe kimya kimya chini ya mapenzi ya
Mungu.
"Huu ndio ujasiri tulio nao kwake, ya kuwa, tukiomba kitu cho chote SAWA SAWA NA MAPENZI YAKE, anatusikia" - (1 Yohana 5:14).
"Huu ndio ujasiri tulio nao kwake, ya kuwa, tukiomba kitu cho chote SAWA SAWA NA MAPENZI YAKE, anatusikia" - (1 Yohana 5:14).
Kumbuka kwamba Mungu anataka
kutufundisha sisi, pamoja na kutupa sisi vitu, kwa njia ya maombi. Kwa hiyo,
wakati mwingine anatuelekeza upande mwingine. Maombi ni njia ya kutusogeza sisi
zaidi na zaidi karibu na mapenzi ya Mungu. Hisia zetu zinatakiwa ziwe kali kutambua
majibu ya Mungu na kujifunza kitu kutokana nayo. Kuyafuatilia kwa karibu maombi
yetu fulani fulani ya pekee pamoja na kile kinachotokea kuhusiana nayo ni
msaada mkubwa kwetu.
Roho Mtakatifu atakusaidia
kulenga shabaha yenyewe: "Roho anawaombea watakatifu kulingana na mapenzi
ya Mungu" (Warumi 8:27. Kumbuka kwamba mapenzi yetu yangeweza kulandana
siku zote na mapenzi ya Mungu endapo sisi tungeweza kuona kama yeye anavyoona.
(4) Mngojee Mungu kwa Saburi.
"NALIMNGOJA BWANA KWA SABURI, akaniinamia akakisikia kilio changu" - (Zaburi 40:1).
"NALIMNGOJA BWANA KWA SABURI, akaniinamia akakisikia kilio changu" - (Zaburi 40:1).
Jambo kubwa hapo ni kukaza
mawazo yako yote kwa Mungu, kukaza mawazo yako yote juu ya suluhisho lake. Wala
usithubutu kumwomba Mungu akusaidie kwa dakika moja, na halafu kujaribu
kuzizamisha shida zako kwa kujifurahisha katika anasa dakika inayofuata.
Umngoje Bwana kwa saburi; tunahitaji kuwa na nidhamu hiyo vibaya sana.
(5) Usiing'ang'anie Dhambi iwayo yote.
("Kama ningalinuia maovu moyoni, Mwenyezi-Mungu hangalinisikiliza")- Zaburi 66:18.
("Kama ningalinuia maovu moyoni, Mwenyezi-Mungu hangalinisikiliza")- Zaburi 66:18.
Dhambi ijulikanayo hukata mara
moja uweza wa Mungu katika maisha yetu; inatutenga mbali na Mungu (Isaya
59:1-2). Huwezi kuishika na kuing'ang'ania dhambi kwa mkono mmoja na kunyosha
mkono mwingine kupokea msaada wa Mungu. Ungamo la dhambi litokalo moyoni hasa
pamoja na toba ya kweli ndilo suluhisho la tatizo hilo.
Kama sisi hatutaki kumruhusu
Mungu kutuweka huru mbali na mawazo, maneno na matendo yetu mabaya, basi,
maombi yetu hayawezi kutuletea jibu lo lote.
"Hata
mwaomba, wala hampati, kwa sababu mwaomba vibaya, ili mvitumie kwa tamaa zenu"
- (Yakobo 4:3).
Mungu hatajibu "ndiyo"
kwa maombi ya uchoyo. Acha wazi masikio yako yapate kuisikia sheria ya Mungu
[Amri Kumi], yaani, mapenzi yake, naye ataacha masikio yake wazi kuzisikia dua
zako.
"Yeye
aligeuzaye sikio lake asiisikie sheria [Amri Kumi], hata sala yake ni
chukizo" - (Mithali 28:9).
(6) Tambua Kwamba Unamhitaji Mungu.
Mungu huwajibu wale wanaoomba kuwako kwake na uweza wake katika maisha yao.
(6) Tambua Kwamba Unamhitaji Mungu.
Mungu huwajibu wale wanaoomba kuwako kwake na uweza wake katika maisha yao.
"Heri
wenye njaa na kiu ya haki, maana hao watashibishwa." - Mathayo 5:6.
(7) Kuendelea Kuomba Tu.
Yesu alitoa kielelezo cha kuwapo kwa haja ya kuendelea tu kutoa dua zetu kwa kusimulia kisa kile cha mjane aliyekuwa anaendelea tu kuomba na kuendelea kuja kwa hakimu akiwa na ombi lake lile, lile. Mwishowe yule hakimu alisema, huku akiwa ameudhika vibaya sana, "Kwa kuwa mjane huyu ananiudhi, nitahakikisha kwamba nampatia haki yake." Kisha Yesu alitoa hitimisho lake hili: "Je! Mungu hatawapatia haki wateule wake wanaomlilia mchana na usiku? Je! atazidi kuahirisha kuwapatia haki yao?" (Luka 18:5-7).

Zungumza na Mungu juu ya
mahitaji yako yote, matumaini yako yote, na ndoto zako zote. Omba mibaraka ya
pekee, omba msaada unapokuwa na shida. Endelea kutafuta, tena endelea tu
kusikiliza, mpaka ujifunze kitu fulani kutokana na jibu lake Mungu.
6. Malaika Wanayahudumia
Mahitaji Ya Waombao
Mtunga Zaburi alishangilia
kwamba kwa njia ya huduma ya malaika wa Bwana maombi yake yalijibiwa:
"Nalimtafuta BWANA akanijibu; akaniponya na hofu zangu zote... malaika wa BWANA hufanya kituo kuwazunguka wale wamchao na kuwaokoa" (Zaburi 34:4-7).
"Nalimtafuta BWANA akanijibu; akaniponya na hofu zangu zote... malaika wa BWANA hufanya kituo kuwazunguka wale wamchao na kuwaokoa" (Zaburi 34:4-7).
Tunapoomba, Mungu anawatuma malaika zake kujibu
maombi yetu (Waebrania 1:14). Kila Mkristo anaye malaika wake mlinzi
anayetembea pamoja naye:
"Angalieni msimdharau mmojawapo wa wadogo hawa. Kwa maana nawaambia ya kwamba MALAIKA WAO mbinguni siku zote huutazama uso wa Baba yangu aliye mbinguni." - Mathayo 18:10.
"Angalieni msimdharau mmojawapo wa wadogo hawa. Kwa maana nawaambia ya kwamba MALAIKA WAO mbinguni siku zote huutazama uso wa Baba yangu aliye mbinguni." - Mathayo 18:10.
Kwa sababu ya maombi yetu tunayotoa:
"Bwana yu karibu. Msiwe na wasiwasi na jambo lo lote, lakini katika kila jambo kwa maombi na dua zetu pamoja na kushukuru, wekeni mambo yenu myatakayo mbele zake Mungu. Ndipo amani ya Mungu, ipitayo ufahamu wote, itawahifadhi mioyo yenu na nia zenu katika Kristo Yesu." - Wafilipi 4:5-7.

7. Mtindo Wa Maisha Ya
Kikristo
Biblia inaeleza wazi juu ya
mtindo wa maisha ya Kikristo. Kulingana na Waefeso 4: 22-24, Mkristo anatakiwa
ku"vua" mtindo wake wa maisha ya zamani uliotokana na "tamaa
zenye kudanganya", na ku"vaa" mtindo mpya wa maisha ambao
ume"umbwa kwa mfano wa Mungu." Katika maandiko hayo na mwongozo
tuligundua kwamba wakati ule wa kuzaliwa upya sisi tuna"umbwa upya"
kuwa watu tofauti ndani ya Kristo.
Mwongozo huu na miongozo sita
inayofuata hutangaza upya mtindo wa maisha ya Mkristo; huifunua siri ya maisha
ya Kikristo yenye furaha. Itakusaidia wewe kujenga uhusiano wenye nguvu zaidi
na Kristo, ambao matokeo yake yatakuwa mtindo wa maisha ya Kikristo ulio
tofauti. Kwa hiyo kaza macho yako kwa Yesu leo hii, nawe unaweza kuwa na sehemu
katika sherehe ile ya mwisho ya ushindi wakati amani yake Kristo itakapotawala
bila kupingwa.