JE! WAJUA KUWA MUNGU ANAKUPENDA?
1. MWENYEZI
MUNGU ANAKUPENDA, NAYE ANATAKA KUKUPANGIA MPANGO WA AJABU KWA MAISHA YAKO.
UPENDO WA
MUNGU
Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili
kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele. Yohana 3:16
MPANGO WA
MUNGU KWAKO
Mimi nalikuja ili wawe na uzima, kisha wawe nao tele. Yohana 10:10
Je,
kwa nini watu wengi hawana uzima huo?
Ni kwa sababu . . .
2. MWANADAMU NI MWENYE DHAMBI. Dhambi zake zimemtenga na
Mungu.Kwa hiyo hajui upendo na mpango wa Mungu kwa maisha yake.
MWANADAMU NI MWENYE
DHAMBI
Kwa sababu wote wamefanya
dhambi, na kupungukiwa na utukufu wa Mungu.Warumi 3:23
Mungu alimwumba mwanadamu kwa
kusudi la kushirikiana naye, lakini mwanadamu alikwenda kinyume cha mpango wa
Mungu. Alichagua kumwasi Mungu badala ya kumtii. Kumwasi Mungu ni kufanya
dhambi. Mtu anapoishi kinyume cha mapenzi ya Mungu anaendelea kuishi maisha ya
dhambi.
MWANADAMU AMETENGANA NA
MUNGU
Lakini maovu yenu yamewatenga
ninyi na Mungu wenu. Isaya 59:2
Mungu Mtakatifu hana ushirika na
dhambi. Kati yake na mwanadamu kuna ufa mkubwa wa dhambi. Mwanadamu hujaribu
kumfikia Mungu kwa nija nyingi: dini, matendo mema, sala, n.k., lakini hizi
zote hazitoshi. Mwanadamu bado ni mwenye dhambi.
Kuna njia moja tu ya
kushirikiana na Mungu . .
3. YESU
KRISTO NI NJIA YA PEKEE YA KUONDOA DHAMBI.
Alikufa kwa ajili yetu ili tujue upendo na
mpango wa Mungu kwa maisha yetu.
ALIKUFA ILI ATULETE KWA MUNGU
Kwa
maana Kristo naye aliteswa mara moja kwa ajili ya dhambi, mwenye haki kwa ajili
yao wasio haki, ili atulete kwa Mungu.1 Petro 3:18
YESU YU HAI
Kristo
alikufa kwa ojili ya dhambi zetu, kama yanenavyo maandiko; na ya kuwa alizikwa;
na ya kuwa alitufuka siku ya tatu, kama yanenavyojil maandiko.1 Wakorintho
15:3,4
YESU NDIYE NJIA YA PEKEE
Yesu
akamwambia, Mimi ndimi njia, na kweli, na uzima; mtu haji kwa Baba, ila kwa
njia ya mimi.Yohana 14:6
Mwanadamu
peke yake hawezi kushirikiana na Mungu. Mungu alimtuma Yesu afe msalabani kwa
ajili ya dhambi zetu na tena awe daraja kati yetu na Mungu ili atulete kwa
Mungu.
Sasa
kanuni ya nne itakuambia jinsi uwezavyo kumjua maishani mwako . . .
4. INAKUPASA
KUMPOKEA YESU AWE MWOKOZI NA MTAWALA WAKO.
Ndipo utajua upendo na mpango wa Mungu kwa
maisha yako.
UNAMPOKEA KRISTO KWA IMANI
Bali
wote waliompokea aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa Mungu, ndio wale
waliaminio jina lake.Yohana 1:12
Kwa
maana mmeokolewa kwa neema, kwa njia ya imani, ambayo hiyo haikutokana na nafsi
zenu, ni kipawa cha Mungu; wala si kwa matendo, mtu awaye yote asije
akajisifu.Waefeso 2:8,9
INAKUPASA KUMKARIBISHA YESU, MAISHANI MWAKO
Tazama,
nasimama milangoni, nabisha, mtu akiisikia sauti yangu, na kuufungua mlango,
nitaingia kwake . . .
Kumpokea
Yesu Kristo ni:
- Kujua
wewe ni mwenye dhambi na kugeuka nafsi yako kwa Mungu na kutubu.
- Kumtegemea
Mungu kwa kukusamehe kabisa.
- Kumkaribisha
Yesu Kristo atawale maisha yako kwa imani, ili uwe kama anavyopenda.
Je,
ni picha gani aliye mfano wa maisha yako?
Je, ni picha gani ambaye ungependa awe mfano wa maisha yako?
Yafuatayo
ni maelezo ya jinsi uwezavyo kumpokea Kristo ndani ya maisha yako?
UNAWEZA KUMPOKEA KRISTO SASA
Mungu
anaufahamu moyo wako. Yafuatayo katika sala hii yanaweza kukusaidia kumpokea Kristo
ukiomba kwa moyo wa kweli.
Bwana Yesu Kristo, ninakuhitaji, mimi ni mwenye dhambi.
Nimekubali kwamba nimejitawala maisha yangu mwenyewe, na kutengana nawe. Asante
kwa kifo chako msalabani kwa ajili ya dhambi zangu na kwa kunisamehe zote. Sasa
nageuka na kutubu. Bwana, nakuomba uingie ndani ya maisha yangu na kunitawala
kabisa. Badili maisha yangu yawe kama upendavyo wewe. Amin.
Je,
sala hii ni sawa na haja ya moyo wako?
Kama
sala hii ni sawa na haja ya moyo wako, basi omba sasa na umkaribishe Kristo
aingie maishani mwako.
YESU YUMO MAISHANI MWAKO
Sasa,
je, umemkaribisha Yesu maishani mwako? Unajuaje?
Kwa hiyo yuko wapi sasa? Kumbuka Ufunuo 3:20.
Yesu alisema ataingia katika maisha yako. Je, si kweli?
Je, unajuaje kuwa Mungu amesikia ombi lako? Mungu ameahidi kwanba lo lote
tuombalo na kuamini litatendeka.
ALIYE NA YESU, ANAO UZIMA WA MILELE
Na
huu ndio ushuhuda, ya kwamba Mungu alitupa uzima wa milele na uzima huu umo
katika Mwana. Yeye aliye naye Mwana, anao huo uzima; asiye naye Mwana wa Mungu
hana huo uzima. Nimewaandikia ninyi mambo hayo, ili mjue ya kuwa mna uzima wa
milele, ninyi mnaoliamini jina la Mwana wa Mungu. 1 Yohana 5:11-13
Umshukuru
Mungu kila siku kwamba Yesu anaishi katika maisha yako.
Uwe na hakika kwamba hatakuacha kabisa. (Mathayo 28:20). Amekupa uzima wa
milele.
USIYATEGEMEE MAWAZO YA MOYO WAKO.
Unaweza
kujisikia leo unalfuraha kisha kesho ukawa na huzuni. Kwa vyovyote
utakavyojisikia Yesu Kristo habadiliki maishani mwako. Waebrania 13:8.
- Ukweli
wa Mungu ndio wenye uwezo wa kutuongoza.
- Tunaunganishwa
na uwezo wa ukweli kwa imani.
- Tunapotii
ukweli, hali ya kujisikia ya moyo (maoni) huongozwa vyema.
- Tunamtegea
Mungu na ukweli wake wala sio hali ya kujisikia ya moyo.
Tukifanya
dhambi tunatubu na yeye anatusamehe.
Basi,
usitegemee mawazo yako, bali utegemee ukweli wa Neno la Mungu kwa imani.
KWA KUWA SASA UMEMPOKEA YESU
Tangu
ulipompokea Kristo mabadiliko mengi yametokea.
- Yesu
ameingia katika maisha yako. (Ufunuo 3:20)
- Umesamehewa
dhambi zako. (Wakolosai 1:14)
- Umefanyika
kuwa mwana wa Mungu. (Yohana 1:12)
- Utazidi
kujua makusudi ya Mungu kwa maisha yako. (2 Wakorintho 5:14,15,17)
Je,
unafikiri kuna jambo lililo bora kuliko kumpokea Yesu katika maisha yako?
Basi,
labda ungependa kumshukuru Mungu sasa kwa vile alivyokurehemu.
Tunathibitisha imani yetu tunapomshukuru Mungu kwa maombi.
Tuombe
tukiwa huru.
Na sasa je?
JINSI YA KUKUA KIROHO
Kama
mtoto mchanga unahitaji kukua
Utaendelea vizuri katika maisha ya kiroho ukiyafuata mashauri yafuatayo kila
siku:
- Zungumza
na Mungu kwa maombi (Yohana 15:7)
- Soma
Neno la Mungu (Matendo 17:11)
- Uwe
mwaminifu kwa Mungu (Yohana 14:21)
- Mshuhudie
Kristo kwa matendo yako na maneno yako (Mathayo 4:19 na Yohana 15:8)
- Umtumaini
Mungu kwa kila jambo katika maisha yako (1 Petro 5:7)
- Umruhusu
Roho Mtakatifu akutawale (Wagalatia 5:16-18 na Matendo 1:8)
NI MUHIMU KWA WAKRISTO KUSHIRIKIANA
Biblia
inatuambia kukusanyika pamoja (Waebrania 10:25)
Ebu,
tutumie mfano wa moto. Kuni nyingi zikirundikwa pamoja zinawaka vizuri sana,
lakini ukiuondoa ukuni mmoja na kuuweka peke yake utapoa. Vile vile wewe haifai
kuishi maisha ya kikristo peke yako.
Ukishirikiana
na watu wengine ambao wamempokea Yesu kuwa Mwokozi wao utazidi kuwa na moto wa
imani.
Uhudhurie
kanisa ambapo watu wanaiamini Biblia kuwa ni kweli na Yesu anatukuzwa.