ATHARI YA DHAMBI
Biblia imeandikwa katika lugha tatu: Kiebrania, Kiarami na Kiyunani. Katika Agano Jipya
neno dhambi limetafsiriwa kutoka neno la Kiyunani ‘hamartia’ likimaanisha kukosea
shabaha (missing the mark). Katika 1 Yohana 3:4, “Kila atendaye dhambi afanya uasi; kwa
kuwa dhambi ni uasi.” Uasi ni kuvuka mstari uliozuiliwa kuvuka. Dhambi imegawanyika
katika mafungu mawili: (1) makatazo, na (2) kutotimiza wajibu. Kwa mfano: Usizini ni
katazo; wakati upendo wa adui ni agizo la kutekeleza.

Katika Marko 10:19-22, tunasoma habari ya Mwanasheria Tajiri Kijana na kuona aina mbili
za uvunjaji wa sheria. Aliweza kujizuia kutovunja karibu makatazo yote. Hakuwahi kuua,
kuzini, kuiba, kushuhudia uongo, kudanganya, n.k. “Akamwaambia, Mwalimu haya yote
nimeyashika tangu utoto wangu. Yesu akamkazia macho, akampenda, akamwambia,
umepungukiwa na neno moja. Enenda ukauze ulivyo navyo vyote, uwape maskini, nawe
utakuwa na hazina mbinguni; kisha njoo unifuate.” Agizo la kutimiza wajibu limetajwa moja
tu, “waheshimu baba yako na mama yako,” lakini amri zote katika fungu hilo ni makatazo.
Biblia pia inaelezea “Kila lisilo la haki ni dhambi…” (1 Yoh.5:17). Katika Kiyunani neno
haki ni “dikaiosune” lenye maana ya tabia ya haki ya Mungu (Warumi 3:5); kama alivyo
mwaminifu, mkweli, n.k. Watu wengi siku hizi huliangalia neno “haki” kwa mtazamo wa
Umoja wa Mataifa (UNO). Lakini Biblia inasema, “…Maana maagizo yako yote ni ya haki”
(Zaburi 119:172). Waisraeli walishutumiwa kwa kutafuta haki zao wenyewe. “Kwa maana
nawashuhudia kwamba wana juhudi kwa ajili ya Mungu, lakini si katika maarifa. Kwa
maana, wakiwa hawaijui haki ya Mungu, na wakitaka kuithibitisha haki yao wenyewe,
hawakujitia chini ya haki ya Mungu” (Warumi 10:1-4). Ikiwa Mungu ndiye aliyetuumba,
hivyo basi ana haki ya kutueleza jambo gani ni la haki na lipi si halali. “Ole wao wasemao
kwamba uovu ni wema, na kwamba wema ni uovu; watiao giza badala ya nuru, na nuru
badala ya giza; watiao uchungu badala ya uchungu!” (Isaya 5:20).
JE, TUNAWEZA KURITHI DHAMBI?
Tunarithi mali, nyumba, n.k. kutoka kwa wazazi, lakini si dhambi. Dhambi inakwenda na
maneno KUTENDA au KUTOTENDA. Lazima mtu afikie umri wa kujua mema na mabaya.
Katika Warumi 7:7 tunasoma, “…Walakini singalitambua dhambi ila kwa sheria; kwa kuwa
singalijua kutamani, kama torati isingalisema, Usitamani.” Watoto wadongo
hawakuhusishwa katika uasi watu wazima Waisraeli. “Tena wadogo wenu, mliosema
watakuwa mateka, na wana wenu, wasio leo na maarifa ya mabaya wala mema, ndio
watakaoingia, nao ndio nitakaowapa, nao wataimiliki” (Kumb.1:39). Kwa kuwa watu
wazima waliwaogopa wenyeji wa Kanaani (wasimwogope Mungu), Mungu aliwaangamiza
wote jangwani kwa miaka 40, isipokuwa Kalebu na Yoshua. Neno la Mungu linasema, “Na
kama yeye [baba mwovu] akizaa mwana, naye [kijana] ameona dhambi zote za baba yake
alizozitenda, akaogopa, asifanye neno lolote kama hayo…hatakufa huyo [kijana] kwa ajili
ya uovu wa baba yake, hakika ataishi” (Ezekieli 18:14-17). Katika mstari 20 tunasoma,
“Roho itendayo dhambi, ndiyo itakayokufa; mwana hatauchukua uovu wa baba yake, wala
baba hatauchukua uovu wa mwanawe, haki yake mwenye haki itakuwa juu yake, uovu wake
mwenye uovu utakuwa juu yake.”
MADHARA YA DHAMBI
Dhambi ina madhara (consequence) makubwa sana! Ndiyo maana Mungu anatusihi sana
tusitende dhambi. Dhambi humwaathiri mtendaji kadhalika watu wengine ambao
hawajaitenda dhambi kama hiyo. Kwa mfano dhambi ya Adamu na Hawa, Biblia inasema,
“Kwa hiyo, kama kwa mtu mmoja dhambi iliingia ulimwenguni, na kwa dhambi hiyo mauti;
na hivyo mauti ikawafikia watu wote kwa sababu wote wamefanya dhambi; maana kabla ya
sheria dhambi ilikuwamo ulimwenguni, lakini dhambi haihesabiwi isipokuwapo sheria;
walakini mauti ilitawala tangu Adamu mpaka Musa, nayo iliwatawala hata wao wasiofanya
dhambi ifananayo na kosa la Adamu, iliyo mfano wake yeye atakayekuja” (Rum.5:12-14).
Katika fungu hilo hapo juu tunaona ni ‘mauti’ iliyowafikia watu wote. Tunakufa ikiwa ni
athari za kosa la Adamu. Kuwa na HATIA (guilt) na kupata MADHARA ni mambo mawili
tofauti. Watu wote wamefanya dhambi, Biblia haifundishi kwamba watu wote wamerithi
dhambi. Ili mtu avunje sheria ni lazima pawe na sheria, kadhalika mtu huyo awe katika umri
ambao atawajibika (accountable).
Hapa nitatoa mifano kubainisha tofauti: Mume aliyeoa halafu akatoka nje ya ndoa na
kuambukizwa virusi vya ukimwi. Kisha akamwambukiza mkewe. Mkewe pia akachukua
mimba na kumwambukiza mtoto aliyezaliwa. Mume, mke na mtoto wote wakafa, je! Mungu
atawahukumu wote hao watatu kwa uzinzi? La! Hasha! Kila mtu atachukua furushi lake
mwenyewe (Wagalatia 6:7). Mwenye hatia ni mume, lakini hao wengine wameathirika kwa
matokeo ya dhambi ya mtu huyo mmoja. Tunakufa si kwa sababu tumerithi dhambi ya
Adamu, bali kutokana na madhara ya dhambi hiyo. Hatuwezi kuupata mti ule wa uzima pale
Bustanini Edeni. Ingekuwa kifo ni ishara ya kuonyesha kwamba mtu ni mwenye dhambi,
basi unapaswa kukumbuka kwamba hata Yesu asiye na dhambi alikufa! (Ebr.4:15).
Mfano mwingine, kiongozi wa serikali fulani ameamua kula rushwa hata Hospitali za umma
kukosa dawa. Unadhani watu wangapi watakufa kutokana na kukosekana kwa dawa katika
hospitali husika? Wengi! Je, wote waliofikwa na mauti kutokana na kukosa matibabu ni wala
rushwa? Jambo ovu tunalolitenda huathiri watoto wetu hata vizazi vingi (Kut.20:4-6).

“ Tazama, mimi naliumbwa katika hali ya uovu; mama yangu alichukua mimba hatiani”
(Zab.51:5). Fungu hili linatumiwa vibaya sana na watu wanaofundisha kwamba watoto
wanazaliwa dhambini. Utata wa sentensi ya kwanza hujibiwa na sehemu ya pili ya fungu hilo
“Mama yangu alichukua mimba hatiani.” Hilo ndilo Daudi analolizungumzia. Mama yake
alichukua mimba katika uzinzi. Watoa maoni wengi wanasema kwamba hapo anazungumzia
ukoo wake ulitokana na zinaa ukiangalia Mwanzo 38:15-30. Yuda alizini na mkwewe Tamari
aliyemzaa Peresi. Kuna vizazi kumi kutoka Peresi hadi Daudi. Mwana haramu hakuruhusiwa
kuingia katika kusanyiko la Bwana (Kumb.23:2). Ndiyo maana tunasoma Daudi akisema,
“Nalifurahia nilipoambiwa, na twende nyumbani kwa Bwana” (Zab.122:1). Katika ukoo huo
Daudi ndiye uzao wa kumi (Angalia Mathayo 1:3-6).
Ukoo wa Daudi uliathiriwa na dhambi ya Yuda, lakini Mungu asingewahukumu kwa dhambi
hiyo. Hata serikali zetu haziwezi kumfunga mtoto kutokana na hatia ya mzazi wake, ingawa
mtoto ataathirika ikiwa mzazi atafungwa gerezani. Mtoto atakosa huduma za mzazi wake
alizokuwa akipewa alipokuwepo. Kuwa na hatia na madhara yatokanyo na dhambi ni vitu
viwili tofauti kabisa. Mungu mwenye haki kuliko serikali dhalimu za duniani hawezi kamwe
kumhesabia mtu hatia kutokana na makosa ya wazazi wake.
Mungu amemwuumba mwanadamu mnyofu, lakini mwanadamu amejivumbulia mavumbuzi
mengi (Mhubiri 7:29). Biblia inasema dhambi huonekana katika mwanadamu katika ujana
wake (Mwanzo 8:21). Kama watoto wangekuwa na dhambi Mungu asingelisema tufanane
nao (1 Kor.14:20; Mt.18:2-4, n.k.).
Asante:

josephmgalula@yahoo.com