Mbunge Mlokole Ataka Jumapili Isitumike Kupiga Kura
Mhe. Asumpta akiwa na Mhe. "Sugu" Wakibadilishana Mawazo.
Mama Mzazi wa Kundi
Maarufu Katika Anga la Muziki wa Injili alimaarufu kama Jsiters.Mbunge
wa Nkenge, Asumpter Mshama (CCM) ameitaka Serikali kutoa tamko la lini
itaacha utaratibu wa kutumia siku ya Jumapili kwa ajili ya kupiga kura.
Mbunge huyo alihoji
iwapo Serikali haioni tatizo kuwadhulumu baadhi ya waumini muda wao na
kwamba jambo hilo limekuwa likisababisha baadhi ya watu kukimbilia
kufanya ibada na huku wakishindwa kupiga kura.
“Kitendo cha
kufanya uchaguzi wa kitaifa siku za Jumapili kinasababisha baadhi ya
watu kushindwa kupiga kura jambo linalowanyima haki yao ya kikatiba,”
alisisitiza Mshama.
Waziri wa Nchi,
Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera Uratibu na Bunge William Lukuvi, alikiri kuwa
sheria za uchaguzi pamoja na kanuni zake, haziainishi siku maalumu ya
iliyoteuliwa kwa ajili ya kupiga kura.
Lukuvi alisema kuwa
uamuzi wa Serikali kuteua siku ya Jumapili kwa ajili ya kupiga kura
ulitokana na sababu kuwa ni siku ambayo Watanzania wengi hawaendi
kufanya kazi hivyo kuwa na fursa katika zoezi la kupiga kura.
Hata hivyo alikiri
kuwa kumekuwa na malalamiko kutoka kwa watu wengi kuhusu siku ya
Jumapili wakitaka ibadilishwe ili isitumike kwa ajili ya kupiga kura
lakini pia Serikali inatambua kwa dhati kuwa ni siku maalumu kwa ajili
ya waumini wa dini ya Kikristo.
Alisema suala hilo
litafanyiwa kazi katika marekebisho ya Katiba Mpya ambayo Tanzania
inatarajia kuipataKatiba Mpya kuanzia Aprili mwakani wakati uchaguzi
mkuu utafanyika Oktoba 2015 .
Source: Mwananchi.
Source: Mwananchi.