UWEZA WA NENO LA MUNGU
Karibuni wapendwa tajadiliane na kushilikishana maneno ya Mungu,
pia kupeana tarifa mbalimbali za kiroho, pia kuombeana ili tuweze
kuishinda dunia hii chafu na kuingia mbinguni yaliko Makazi sahihi na ya
milele.
hakuna mtu anayebanwa uhuru ni wako hubiri kadri uwezavyo, omba ushuri, au ombea wanzako .
kwa wachungaji au mtu nayetaka kuweka mahubiri yake kwenye eneo
hili na akapata tatizo kama la kushindwa kuweka ujumbe wake... asisite
kuwasiliana nami kwa kupitia email hii. embackgrace@hotmail.com
UMUHIMU WA KUJUA NENO LA MUNGU
Na Mwinjilisti Simon Mkanza
Upo umuhimu wa kujua neno la Mungu katika maisha ya Mkristo halisi.
Biblia inatuambia Yesu Kristo ndiye Neno la Mungu. Kwa maneno mengine Yesu ndiye Neno ambalo Mkristo anapaswa kuwa nalo (Yohana 1:1).
Kwa kusema hivyo kuna umuhimu wa kumjua Yesu na kumshika, kwa
maana yeye ndiye Neno la Mungu. Katika Biblia mtume Petro anasema
mbele za Yesu kwamba, twende kwa nani na wewe ndio mwenye maneno ya
uzima? Petro alijua upo umuhimu wa kumjua Yesu kama Neno maana ndani ya Neno kuna uzima
|
|
|
Biblia inasema neno la Kristo likae kwa wingi ndani yetu (Wakolosai 3:16).
Kwa nini basi neno la Kristo likae kwa wingi ndani yetu? Ni kwa
sababu lina mambo yafuatayo ambayo ni muhimu katika maisha yetu ya
Ukristo. Mambo hayo ni…
A) Neno la Mungu li Hai
B) Neno la Mungu lina nguvu (Mwanzo 1:6).
C) Neno la Mungu lina ukali kuliko upanga
D) Neno la Mungu linachoma hata kuzigawanya nafsi, roho viungo na mafuta yaliyomo ndani yake
E) Neno la Mungu li jepesi kuyatambua mawazo na makusudi ya moyo
KWA NINI NENO LA MUNGU LI HAI?
Neno la Mungu li hai kwa sababu Mungu mwenyewe analithibitisha kwamba li hai maana
a) Linafanya mabadiliko (Isaya 55:10-11).
b) Linatupa kushinda dhambi (Zaburi 119:11).
c) Neno la Mungu li hai kwa sababu linatupa mafanikio katik
mwili. Petro anasema ”kwa neno lako tunatupa nyavu zetu.“ Hapa
tunaona kuwa Neno la Mungu pekee yake ndilo linaloweza kuleta majibu
katika maisha yetu (Luka 5:3-6).
Uhai wa Neno la Mungu kwa mtu ndio unaoleta kushinda dhambi. Nao wakamshinda kwa neno la ushuhuda wao (Ufunuo 12:11).
Daudi aligundua au kwa maneno mengine alifahamu umuhimu wa neno la Mungu katika maisha, kama vile mtume Paulo anavyosema na Wakolosai kwa habari ya neno la Kristo kwamba likae kwa wingi ndani ya mioyo yetu
Neno la Mungu lina nguvu na ndio maana tunamshinda shetani kwa neno la Mungu.
Yesu kama kielelezo yeye mwenyewe ni neno ndani ya neno anamshinda shetani (Luka 4:1-12).
Katika mistari hiyo tunaona Yesu anamwambia shetani
”imeandikwa“ Shetani nae anageuza usemi nae anamwambia Yesu
”imeandikwa kwamba atakuagizia malaika usije ukajikwaa mguu wako.“ Kwa
kuwaYesu neno la Mungu limo ndani yake hamwambii tena shetani
imeandikwa ila anamwambia imenenwa. Kwa maneno mengine tukiwa na neno
la Yesu ndani yetu hatuwezi kuyumbishwa. Kwanini? Kwa sababu
tumeshaona jinsi ambavyo shetani anajaribu kutumia neno la Mungu
kwa kusema ”imeandikwa.“ Na ni kweli imeandikwa ananukuu kutoka
kitabu cha Zaburi 91 :1-12. Hata kama shetani ananukuu maandiko haina
sababu yamimi kushindwa na shetani maana Yesu tayari alikwisha
mshinda. Yesu kumshinda shetani ina nipelekea mimi kusoma neno la
Mungu kwa bidii sana.
Kwa mfano, ni kweli kabisa imeandikwa mtakula vitu vya kufisha
havitawadhuru lakini je, ninywe sumu sitakufa kwa sababu imeandikwa?
Hapana, ukinywa hakika utakufa. Shetani hutumia mandiko kuwafunga
wasiojua neno la KristoYesu.
Katika Biblia tunasoma pia kwamba ”imeandikwa“ Wanandoa MKE na
MUME wasinyimane. Kwa kutojua neno vijana wa kiume na wa kike
wamedanganywa. Si hao tu hata walioko kwenye ndoa wametegwa kwa andiko
hilo. Neno linasema katika Mithali 6:32
”Aziniye na mwanamke hana akili kabisa“ na Mwanamke vivyo hivyo
akizini na mwanaume hana akili kabisa. Watu wamepata hasara ya mambo
mengi kwa kutojua neno la Mungu. Ili
tuweze kumshinda shetani ni lazima neno la Yesu liwe ndani yetu
ndiposa tutamshinda shetani. Ayubu kwa neno la Mungu alishinda. (Ayubu 19:25-27, Waefeso 6:17).
Nataka nikwambie neno la Mungu ni msaada katika maisha yetu maana hutupa majibu ya maisha yetu. Katika Luka 5:3-6
tunasoma jinsi Petro na wenzake walivyopata samaki wengi kwa kutii
neno la Kristo. Kumbuka pia juu ya yule akida, alimwambia Yesu
”...sema neno tu na mtumwa wangu atapona“ (Luka 7:2-10). Yesu akisema neno lazima mabadiliko yatokee.
Neno la Mungu lina ukali kuliko upanga.
Kwa nini neno la Mungu lina ukali kuliko upanga? Upanga unaweza
kukukata na usipone. Lakini neno linakata na kuponya. Kwa neno hili
wafalme wanatubu. Yona alitumia neno la Mungu likawa kali watu
wakatubu. (Yona 3:1-10; Matendo ya Mitume 8:18-24).
Neno la Mungu linachoma hata kuzigawa nafsi na roho na viungo na mafuta yaliyomo ndani yake (Matendo 7:51-54, Yohana 4:16 -18, 27-29). Mwanamke akaambiwa mambo yake; Neno likachambua kila tabia..
Neno la Mungu li jepesi kutambua mawazo na makusudi ya moyo.
Yesu kama Neno la Mungu anajua mambo ambayo watu wanawaza ndani ya mioyo yao (Luka 5:17-24, 6:6-8 ; Mathayo 16:1-4). Yapo makusudi ya moyo ambayo ni ya siri sana kwa mwanadamu lakini nataka nikuambie neno la Mungu ni jepesi kutambua makusudi ya moyo.
Mtume Petro aliyependa kujua neno la Mungu, naye pia Mungu alimjalia neema ya kuyajua makusudi ya moyo wa mwanadamu (Matendo 5:1-11).
Elisha aliyajua makusudi ya moyo wa mfalme ya kuwatenda Israeli kwa
siri ila Mungu alimpa neema ya kuyajua mawazo ya mfalme (2 Wafalme 6:8-12).
Hili ni jambo la msingi katika maisha ya Mkristo yaani kulijua
neno la Mungu. Neno la Mungu tukiwa nalo na likitenda kazi ndani yetu
lazima tufanikiwe (Yoshua 1:8) .
Je unahitaji kuwa na imani katika neno la Mungu? Basi, ni neno
la Mungu peke yake ambalo laweza kuumba imani, maana pasipo neno la
Mungu hakuna imani (Waebrania 11:3 ; Warumi10:17). Ili uwe mwanafunzi wa Yesu ni lazima ulijue neno la Mungu na kulishika.(Yohana 8:31 ; Luka 2:19).
Kama neno halimo ndani yetu tunayoyafanya yanakuwa hayana Mungu, hata
twaweza kusalitiana. Mtu anayelitamani neno la Yesu huling’ang’ania
na kulitenda maana kwake ni nguvu. (1Wakorintho 1:18). Si kwamba Neno la Mungu ni nguvu tu: bali huleta faida (Mathayo 13:23).
Watu wengi tunapotea kwa kutokujua uwezo (nguvu) iliyomo katika neno la Mungu (Mathayo 22:29).
Yesu anasema, mtu anayelitenda neno la Mungu na kulishika huyo
amepanda mbegu ambayo itazaa sana, maana ndani ya moyo wake imo mbegu
ambayo ni neno la Mungu la uponyaji na mafanikio, msamaha, utu wema na
mengi yanayofanana na hayo.
Yapaswa maisha yetu yawe yenye neno (mbegu) la Mungu ili tuweze kuzaa mambo mazuri.
Wokovu wetu unaimarika kwenye neno la Mungu. Hilo neno la Mungu tunalipata wapi? Isaya 34:16. Upo umuhimu wa kuyachunguza maandiko ili kujua Mungu anasema nini (Matendo 17.10-11). Je, tangu ulipowekwa msingi wa wokovu, neno limo ndani? (Hagai 2:18-19). Kila kitu kinaweza kupita lakini sio neno la Mungu (Isaya 40:8, Mathayo 24:35).
Ili neno litende
kazi katika kinywa chako unapolitamka na kuamini ni lazima iwepo nguvu
ya Roho Mtakatifu. Bila hii nguvu hamna kitakacho endelea. Utasema
umeamini lakini hakutakuwa na matokeo. Mungu mwenyewe alipotamka neno
liliambatana na nguvu ya Roho Mtakatifu (Mwanzo1:2-3).
Mungu akubariki |