Ni katika bweni la KIMWERI mwizi huyo amekamatwa na kupewa kichapo kitakatifu na wanafunzi wenzake. Baada ya kichapo hicho mwizi huyo ameachiwa na kukimbilia uwanja wa mpira uliopo magharibi mwa chuo hicho alimaarufu kama valley. Pamoja na kuachiliwa kwake bado kuna waliowahi kuibiwa bila kujali ni nani aliwaibia waliendelea kumfuata na kumkamata kumkamata kumpa kichapo cha aina ileile na kisha kumfikisha kituo cha polisi kilichopo maeneo ya Mzumbe Changalawe.
Mwizi huyo inasemekana alikuwa ni mwanafunzi wa BBA Marketing mkazi wa mkoani Mbeya lakini ali- DISCO kipindi cha muhula wa pili mwaka wa kwanza. Hii imekuwa ni tabia ya wanafunzi wengi wa vyuo vikuu inapofika mahali wamefeli hawataki kukubaliana na matokeo na hatimaye kurudi chuoni bila kuwafahamisha wazazi wao nyumbani. ,