DHAMBI YA UZINZI NA HATARI ZAKE:
SEHEMU YA KWANZA
Nakusalimu
katika jina la Bwana mwezi huu wa tisa. Katika mwezi huu nimesukumwa ndani
yangu tujiunze habari hii juu ya athari/matokeo ya dhambi ya zinaa/uasherati
pale kwa mtu aliyeokoka. Yaani kitu gani kinatokea mtu aliyekwisha
kuokoka anapoanguka katika dhambi hii.
Katika
Mithali 6:32 Biblia inasema “Mtu aziniye na mwanamke hana akili kabisa; afanya
jambo litakalomwangamiza nafsi yake” na pia katika Mithali 6:26 inasema
“Maana kwa Malaya mtu hutiwa katika hali ya kuhitaji kipande cha mkate; na
kahaba humwinda mtu anase nafsi yake iliyo ya thamani”
Ni
watu wengi sana ambao wamerudi nyuma na kuanguka katika dhambi hii, wapo ambao
kwa hiari yao walikuja kwangu moja kwa moja niweze kusaidiana nao katika hili,
wapo wengine ambao hata wao pasipo kuniambia walilofanya Mungu alifunulia na
kunionyesha jinsi watu hao walivyoanguka katika dhambi hii na madhara yake.
Hadi sasa bado kuna kundi kubwa la watu waliokoka ambao bado dhambi hii ina
nguvu juu yao na bado wanafanya jambo hili kinyume na mapenzi ya Mungu katika
maisha yao.
Si
kana kwamba Mungu anafuga dhambi kwa kutokuwadhihirisha hao watu na uovu wao,
isipokuwa hataki jina lake litukanwe, kwa kuwa ikijulikana huyo mtu au hao watu
wameanguka huenda kutokana na nafasi zao kiuongozi, kihuduma kiushuhuda
nk jina la Mungu litatukanwa sana na mataifa lakini pia hata na wale
waliokwisha kuokoka. Kwa lugha rahisi hao watu au huyo mtu atakuwa ametoa
nafasi ya jina la Mungu kutukanwa.
Kwa
bahati mbaya sehemu kubwa ya watumishi wa Mungu katika makanisa yao wanoona
athari ya hili jambo katika upana wakekama Biblia inavyosema.
Inafika mahali baadhi yao wanawafariji wale walioanguka kwa kusema jipe
moyo, tubu na Mungu ni wa rehema atakusamehe. Na wengine utasikia wanasema
haukuanza wewe, Daudi naye yalimshinda sembuse wewe.
Wengine
wanatumia maandiko kabisa wanasema mwenye haki huanguka mara saba, we mara moja
tu wala isikusumbue sana tengeneza tu Mungu atakusamehe, na wengine wanasema
mimi mwenyewe nilishindwa so, hata wewe isikusumbue sana kazana tu uoe wa kwako
au omba upate mume. Ni kama vile watu wanatumia rehema/neema ya Mungu kuendelea
kutenda dhambi (It seems as if people are taking the advantage of God’s mercy/grace
to commit sin).
Si
kana kwamba napingana na neno au na mawzo ya hao watumishi wenzangu. Nakubali
kwamba Mungu husamehe dhambi na maovu ikiwa ni pamoja na dhambi hii
ya uasherati/uzinzi. Mungu husamehe kwa sababu moja hafurahii kifo cha mwenye
dhambi na pili ni ili kukurejesha kwenye nafasi yako ili uweze kulitumikia
kusudi lake. Lakini je, unajua madhara/matokeo ya dhambi hii kwa mtu
aliyeokoka anapoifanya? Hata kama akikusamehe/amekusamehe, unajua nini
kimetokea/kilitokea kwako pale ulipofanya dhambi hii? Au je unaijua gharama ya
kurejea kwenye nafasi yako aliyoikusudia Mungu?
Katika
miaka zaidi ya sita niliyomtumikia Mungu nimejifunza na kukutana na kesi nyingi
sana za watu mbalimbali katika suala hili. Kwa hiyo ninapoandika haya si
tu maadamu naweza kuandika ila naandiaka vitu ninavyojua vinatokea kweli na
athari yake ikoje. Na mwezi huu wa tisa ndio kitu ambacho nasikia rohoni
tujifunze kwa pamoja.
Biblia
inasema aziniye na mwanamke afanya jambo litakalomwangamiza nafsi yake? Huenda huwa unausoma tu huo msitari
bila kujua uzito wa hayo maneno. Ni vizuri kwanza ukajua kwamba ndani ya nafsi
ya mtu ndiko kwenye hisia, nia, akili, na maamuzi.
Mambo
matatu yafuatayo ndiyo yanayotokea mtu aliyeokoka anpofanya dhambi hii ya
uasherati/zinaa ;
Moja,
Kuharibika kwa mfumo wa mahusiano na mawasiliano kati yake na Mungu.
Katika
mfumo wa ufalme wa Ki – Mungu ni kawaida kwa mtu aliyeokoka na mwenye mahusiano
mazuri na Mungu, kuona Mungu akiwasiliana naye kwa njia mbalimbali ili
kumshirikisha mawazo na mipango yake ikiwa ni namna ya kumuongoza mtu huyo
katika kusudi lake chi ya jua. Hii ina maana suala la mawasiliano kati ya
mtu na Mungu ni la kawaida kwa mtu mwenye mahusiano mazuri na Mungu wake.
Sasa
mtu anapofanya dhambi hii, athari yake ni hii, dhambi inaharibu mfumo huu wa
mahusiano kati ya mtu na Mungu. Na mahusiano kati ya mtu na Mungu
yakiharibika mawasilano kati ya Mungu na mtu yanakatika/kuharibika pia.
Ninaposema yanakatika ina maana si rahisi kwa Mungu kusema tena na huyo mtu au huyo
mtu kusema tena na Mungu wake kwa sababu asili/mazingira ya mfumo huu
hayaruhusu na hili linapelekea mafunuo/sauti ya Bwana kuwa hadimu kwako, kwa
kanisa, kwa jamii, kwa kampuni na hata nchi tegemeana na nafasi yako katika
ufalme wa Mungu.
Pili,
Kuharibika kwa mfumo wa kufanya maamuzi/kufikiri ndani yako.
Dhambi
hii inaharibu mfumo wa kufanya maamuzi, shetani anapomuongoza mtu kufanya
dhambi hii, lengo/interest yake ipo kwenye nafsi ya mtu huyo. Shetani akikamata
nafsi ya mtu maana yake amekamata akili/nia ya mtu huyo, akikamata akili ya mtu
huyo maana yake amekamata maamuzi yake pia. Na akikamata maamuzi
yako amekamata matokeo ya maisha yako ya sasa na ya baadae.
Hivyo
mtu huyu hataweza tena kufikiri mambo ya rohoni kama Paulo anavyoagiza
kwa Warumi ile sura ya 8:5 “Kwa maana wale waufuatao mwili huyafikiri mambo
ya mwili, bali wale waifuatao roho huyafikiri mambo ya roho. Hivyo kufanya
dhambi hii ni kuathiri mfumo wako wa kufanya maamuzi, na hii ina maana hata
Mungu akileta wazo lake kwako huwezi kulipokea maana mfumo wa kuamua
umeukabidhi kwa Shetani kwa njia ya zinaa/uasherati.
Tatu,
Kuharibika kwa mfumo wa utiifu ndani yako.
Warumi
2:13 says ‘Kwa sababu sio wale wasikiao sheria walio wenye kuhesabiwa
haki, bali ni wale waitendao sheria watakaohesabiwa haki”. Kuharibika
kwa mifumo huu huu, ni matokeo ya kuharibika kwa mifumo miwili hapo juu yaani
ule wa mahusiano na ule wa kufanya maamuzi. Ubaya wa dhambi hii inaharibu
mifumo hii ambaayo ndiyo misingi ya mwenye haki. Fuatili maisha ya watu wengi
sana walioanguka kwenye dhambi hii angalia utiifu wao mbele za Mungu ukoje.
Nakuhakikishia utagundua ni ngumu sana kwao kutii maagizo ya Mungu kwao. Mtu wa
aina hii hata Mungu akimpa maagizo ya kutekeleza hataweza kwa kuwa tayari
mahusiano yamevunjika, mamuzi yametekwa .
Nini
Mungu anataka tujifunze katika hili?
Unapokuwa
na mahusiano mazuri na Mungu hii mifumo yote mitatu inafanya kazi vizuri.
Dhambi hii inapoingia inasababisha kuharibka kwa mifumo hii mitatu. Kitu kibaya
au kinacho muumiza Mungu ni kwamba hata kama akikusamehe pale
utakapotubu, kwa sababu hii ni mifumo itakugharimu sana kuirejesha mahali pake.
“It will cost you taking the systems back to the ancient paths”. Na ndio
maana neno linasema afanya jambo litakalomwangamiza nafsi yake. Hii ina maana
kila kilichomo ndani ya nafsi pia kinaangamizwa. Ili kuirejesha mifumo hii
maombi ya muda mrefu ya rehema na kutengeza mahali palipobomoka ni ya
lazima.
Yamkini
unaweza kusema la muhimu Mungu amenisamehe, hayo mengine sijali sana.Unaweza
kusema hayo maneno kama hujui/ huelewi muda unathamani kiasi gani kwa Mungu, na
pia mahusiano kati ya muda na Mungu. Ngoja nikuambie siri ya Mungu na muda japo
kidogo. Muda na Mungu ni marafiki, na tena wote wana mahusiano mzuri sana.
Muda anaongoza maamuzi ya Mungu na Mungu anaongoza matumizi ya muda kwa kuiweka
mipango katika ndani ya mtu na kumwagiza atekeleze ndani ya muda. Hivyo kwa
Mungu muda ni muhimu sana.
Kitu
gani namaanisha hapa;
Mungu
hakutenga/kuweka muda wa mtu kurejesha mifumo hii kwa sababu umeanguka katika
dhambi. Katika kipindi ambacho wewe unatubu na kutengeneza kwa Mungu wako ili
kurejesha mifumo hii, basi uwe na uhakika upande wa pili umesha athiri kusudi
la Mungu duniani kupitia wewe. Sasa kama utatumia siku tano, mwezi mmoja,
miezi sita, mwaka mzima nk, kurejesha hii mifumo basi kwa kipindi hichocho
utakuwa umekwamisha kusudi la Mungu kupitia wewe. Na ndio maana biblia inasema
Shetani anawinda nafsi yako iliyo ya thamani, maana anajua akikamata nafsi yako
amekamata akili, nia, hisia na maamuzi yako na hivyo amefanikiwa kuharibu hiyo
mifumo na kusababisha mipango ya Mungu isifanyike kwa muda aliokusudia kupitia
wewe.
Labda
tujifunze kwa mfano huu;
Fikiria
umepangiwa na Mungu kusafiri umbali wa kilomita 500 ndani ya masaa saba (7).
Mungu amekupa gari ambalo ni kusudi lake kwako. Hivyo
litazame gari ulilopewa kama kusudi la Mungu kwako na wewe ni
dereva. Sasa wewe ukaamua kuliendesha gari bila kuweka maji kwenye
injini. Baada ya kusafiri umbali wa kilomita 300 injini ya gari ikafa kwa
kukosa maji na mbele yako zimebaki kilomita 200. Je unajua utakuwa umeathiri
kwa kiwango gani kusudi la Mungu?. Kutokana na mfano huu unapotenda dhambi hii
je unajua ni kwa kiwango gani utakuwa umeathiri mipango ya Mungu kupitia
wewe duniani kwa kipindi chote ambacho utakuwa unairejesha mifumo mahali pake?.